Author
Listed:
- Pius M Mwanza
- Dkt Sarah Ngesu
- Dkt F. M. Musyoka
Abstract
Lengo la Utafiti:Utafiti huu ulinuia kutathmini nyimbo za Kiswahili zinazotumika katika shule za chekechea kama nyenzo ya ufundishaji katika kata nne za Kaunti ya Makueni ambazo ni Mukaa, Kilungu, Kathonzweni na Makueni. Madhumuni ya utafiti huu ilikuwa ni;Mosi, kuainisha aina za nyimbo za Kiswahili zilizotumika kama nyenzo ya ufundishaji katika shule za chekechea nchini Kenya.Pili, kubainisha namna nyimbo za Kiswahili zilivyotumika kama nyenzo ya ufundishaji.Tatu, kufafanua athari za matumizi ya nyimbo za Kiswahili kama nyenzo ya ufundishaji katika shule za chekechea. Mbinu za Utafiti:Kaunti ya Makueni ina idadi ya kata tisa kwa ujumla. Kata hizi nne ziliteuliwa kwa sababu utafiti wa awali ulionyesha kwamba kwenye kata hizo kuna shule za chekechea ambazo zina mchanganyiko wa walimu na wanafunzi kutoka maeneo mbalimbali nchini Kenya na waliozungumza lugha asili tofauti.Shule saba za kiserikali na tatu za kibinafsi ambazo zenye wanafunzi wengi zilishughulikiwa katika utafiti huu. Shule mbili hadi tatu zilichaguliwa katika kila kata kulingana na idadi ya wanafunzi na maeneo ya shule hizo.Mbinu ya kusudio ilitumika kuchagua nyimbo za Kiswahili ishirini na tano kwa jumla. Sampuli lengwa ilikuwa ni shule saba za kiserikali na tatu za kibinafsi. Pia, mbinu ya hojaji ilitumika katika ukusanyaji wa data kutoka kwa walimu.Data ya utafiti huu ilichanganuliwa kwa kutumia njia ya kimaelezo na kitakwimu.Utafiti uliongozwa na nadharia ya kiutambuzi iliyoasisiwa na Jean Piaget mwaka wa 1954. Matokeo ya Utafiti:Utafiti huu umebaini kwamba nyimbo za Kiswahili ni mojawapo ya nyenzo muhimu ya ufundishaji katika shule za chekechea nchini Kenya. Mchango wa Kipekee kwa Nadharia, Sera na Mazoezi:Kwa Nadharia:Utafiti uliongozwa na nadharia ya kiutambuzi iliyoasisiwa na Jean Piaget mwaka wa 1954.Kwa Sera:Nyimbo za Kiswahili zilitumika katika ufundishaji katika sehemu kubwa kwa kuwa zilieleweka na wanafunzi wote.Kwa Mazoezi:Nyimbo za Kiswahili zinazotumika katika shule za chekechea kama nyenzo ya ufundishaji.
Suggested Citation
Pius M Mwanza & Dkt Sarah Ngesu & Dkt F. M. Musyoka, 2025.
"Tathmini ya Nyimbo za Kiswahili Kama Nyenzo ya Ufundishaji Katika Shule za Chekechea,"
European Journal of Linguistics, CARI Journals Limited, vol. 4(3), pages 1-18.
Handle:
RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:3:p:1-18:id:3084
Download full text from publisher
Corrections
All material on this site has been provided by the respective publishers and authors. You can help correct errors and omissions. When requesting a correction, please mention this item's handle: RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:3:p:1-18:id:3084. See general information about how to correct material in RePEc.
If you have authored this item and are not yet registered with RePEc, we encourage you to do it here. This allows to link your profile to this item. It also allows you to accept potential citations to this item that we are uncertain about.
We have no bibliographic references for this item. You can help adding them by using this form .
If you know of missing items citing this one, you can help us creating those links by adding the relevant references in the same way as above, for each refering item. If you are a registered author of this item, you may also want to check the "citations" tab in your RePEc Author Service profile, as there may be some citations waiting for confirmation.
For technical questions regarding this item, or to correct its authors, title, abstract, bibliographic or download information, contact: Chief Editor (email available below). General contact details of provider: https://www.carijournals.org/journals/index.php/ejl/ .
Please note that corrections may take a couple of weeks to filter through
the various RePEc services.