IDEAS home Printed from https://ideas.repec.org/a/bhx/ojtejl/v4y2025i2p49-67id2936.html
   My bibliography  Save this article

Uchanganuzi Linganishi wa Usawiri wa Wahusika wa Kiume Katika Riwaya ya Kiswahili

Author

Listed:
  • Dorcas Kasiva Kimondiu
  • Dr. Francis Musyoka
  • Dr. Esther Chomba

Abstract

Makala haya yanakusudia kuchanganua na kulinganisha wahusika wa kiume katika riwaya teule za Kiswahili ambazo ni: Mwisho wa Kosa, (1987) iliyoandikwa na Zainabu Burhani, Siku Njema (1996), iliyoandikwa na Ken Walibora, Taswira za Mawingu, (2011) iliyoandikwa na Sinjiri Mukuba na Nguu za Jadi, (2021) iliyoandikwa na Clara Momanyi. Makala haya yanaegemea nadharia ya Mwanamume Mpya. Nadharia hii iliasisiwa na Beynon (2002). Nadharia ya Mwanamume Mpya inajaribu kueleza kwa nini baadhi ya wanaume hukaa na wake zao kwa usawa bila kuonesha tabia za mfumo dume ambazo huashiria kuwepo kwa taasubi ya kiume. Mihimili ya nadharia ya Mwanamume Mpya iliyoongoza makala haya ni kusaidia wake zao na wanawake wengine katika jamii kujiendeleza kielimu na kikazi, kukubali majukumu yoyote ya kiuana bila kujali jinsia au watu wanaomzunguka, kutoonesha udikteta katika familia zao pamoja na jamii inayowazunguka, kuwaona wanawake kama viumbe sawa na wanaume kwa kuwaheshimu na kuwapenda katika kila nyanja wanazokuwepo na kukosoa nafsi zao na mazoea yao kama wanaume. Mbinu ya Fasihi Linganishi imetumika kulinganisha na kulinganua usawiri wa wahusika wa kiume katika riwaya teule. Data iliyotumika katika Makala haya ilitolewa maktabani. Maktabani, tasnifu, makala na vitabu vinavyohusiana na mada vilisomwa kwa kina. Uwasilishaji wa matokeo umefanyika kwa njia ya maelezo na michoro faafu. Matokeo yameonesha kuwa waandishi wa kike wamemsawiri mwanamume kwa mtazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa kiume. Kwa hivyo, kulingana na waandishi wa kike mwanamume ni mpya. Kulingana na mpito wa wakati waandishi wa karne ya ishirini wamemsawiri mhusika wa kiume kwa mitazamo chanya ikilinganishwa na waandishi wa karne ya ishirini na moja. Kwa hivyo mwanamume ni mpya kulingana na waandishi wa karne ya ishirini.

Suggested Citation

  • Dorcas Kasiva Kimondiu & Dr. Francis Musyoka & Dr. Esther Chomba, 2025. "Uchanganuzi Linganishi wa Usawiri wa Wahusika wa Kiume Katika Riwaya ya Kiswahili," European Journal of Linguistics, CARI Journals Limited, vol. 4(2), pages 49-67.
  • Handle: RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:49-67:id:2936
    as

    Download full text from publisher

    File URL: https://carijournals.org/journals/index.php/ejl/article/view/2936
    Download Restriction: no
    ---><---

    More about this item

    Keywords

    ;
    ;
    ;
    ;
    ;

    Statistics

    Access and download statistics

    Corrections

    All material on this site has been provided by the respective publishers and authors. You can help correct errors and omissions. When requesting a correction, please mention this item's handle: RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:49-67:id:2936. See general information about how to correct material in RePEc.

    If you have authored this item and are not yet registered with RePEc, we encourage you to do it here. This allows to link your profile to this item. It also allows you to accept potential citations to this item that we are uncertain about.

    We have no bibliographic references for this item. You can help adding them by using this form .

    If you know of missing items citing this one, you can help us creating those links by adding the relevant references in the same way as above, for each refering item. If you are a registered author of this item, you may also want to check the "citations" tab in your RePEc Author Service profile, as there may be some citations waiting for confirmation.

    For technical questions regarding this item, or to correct its authors, title, abstract, bibliographic or download information, contact: Chief Editor (email available below). General contact details of provider: https://www.carijournals.org/journals/index.php/ejl/ .

    Please note that corrections may take a couple of weeks to filter through the various RePEc services.

    IDEAS is a RePEc service. RePEc uses bibliographic data supplied by the respective publishers.