IDEAS home Printed from https://ideas.repec.org/a/bhx/ojtejl/v4y2025i2p1-17id2783.html
   My bibliography  Save this article

Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili

Author

Listed:
  • Mutisya Cosmas Mbithi
  • Dr. Sarah Ndanu Ngesu
  • Dr. Esther N. Chomba

Abstract

Kusudi: Utafiti huu ulichunguza usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia katika vitabu vya Kiingereza vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Utafiti huu ulidhamiria kuchunguza na kubainisha usahihi wa uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia kutoka kiswahili lugha isiyo na viwakilishi bainifu vya jinsia kwenda kiingereza lugha yenye viwakilishi bainifu ya jinsia. Mbinu: Data za utafiti zilipatikana kwa kusoma, kuchanganua na kuhakiki tafsiri ya vitabu teule vya fasihi: Siku Njema ya Walibora (1996) na tafsiri yake A Good Day iliyotafsiriwa na Kweyu na Kawegere (2019), Kaburi bila Msalaba iliyoandikwa na Kareithi (1969) na tafsiri yake ya Kiingereza Unmarked Grave iliyotafsiriwa na Githiora (2017). Vilevile, mtafiti aliangazia tamthilia mbili; Tamthilia ya Natala iliyoandikwa na Mberia (1997) na tafsiri yake ya Kiingereza Natala iliyotafsiriwa na Kasu na Marami (2011). Tamthilia ya Kinjekitile iliyoandikwa na Hussein (1969) na tafsiri yake Kinjekitile iliyotafsiriwa na Hussein mwenyewe (1970) ilichunguzwa. Mtafiti aliteua vitabu hivi kwa kuwa vilionesha utajiri wa data inayohusu uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia. Utafiti huu uliongozwa na Nadharia ya Skopos na Nadharia ya Usawa wa Kidhima. Nadharia ya Skopos iliyoasisiwa na Hanns Vermeer (1978) ambayo husisitiza kuwa, kimsingi kutafsiri kunafaa kushughulikia jukumu la matini chanzi na matini lengwa yaani tafsiri ni kitendo chenye malengo. Nadharia ya Usawa wa Kidhima iliasisiwa na Nida (1964) na inatilia mkazo usawa wa kimaana na athari sawa kwa hadhira katika mchakato wa tafsiri. Baada ya kubainisha uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, data hiyo ilichanganuliwa kitaamuli na kitakwimu na matokeo kuwasilishwa kupita maandishi ya kinadhari majedwali na michoro ya miche duara kutathimini usahihi uhawilishaji huo. Matokeo: Matokeo ya utafiti huu yanaonesha kuwa wafasiri wa vitabu teule wamehawilisha viwakilishi vya jinsia kwa usahihi na uhawilishaji mwingine ukazua utata. Uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia unachangamoto nyingi kwa hivyo wafasiri wanapaswa kumakinika kwani, uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia huwa na athari asi na chanya kwa hadhira lengwa. Mchango wa kipekee kwa nadharia, vitendo na sera: Utafiti huu unapendekeza utafiti zaidi kufanywa katika uhawilishaji wa viwakilishi vya nyakati katika tafsiri kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza kwani kama uhawilishaji wa viwakilishi vya jinsia, uhawilishaji wa viwakilishi vya wakati vilevile, vinaweza kuwa na athari kwa ujumbe asilia.

Suggested Citation

  • Mutisya Cosmas Mbithi & Dr. Sarah Ndanu Ngesu & Dr. Esther N. Chomba, 2025. "Usahihi wa Uhawilishaji wa Viwakilishi vya Jinsia katika Vitabu vya Kiingereza Vilivyotafsiriwa kutoka Kiswahili," European Journal of Linguistics, CARI Journals Limited, vol. 4(2), pages 1-17.
  • Handle: RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:1-17:id:2783
    as

    Download full text from publisher

    File URL: https://carijournals.org/journals/index.php/ejl/article/view/2783
    Download Restriction: no
    ---><---

    Corrections

    All material on this site has been provided by the respective publishers and authors. You can help correct errors and omissions. When requesting a correction, please mention this item's handle: RePEc:bhx:ojtejl:v:4:y:2025:i:2:p:1-17:id:2783. See general information about how to correct material in RePEc.

    If you have authored this item and are not yet registered with RePEc, we encourage you to do it here. This allows to link your profile to this item. It also allows you to accept potential citations to this item that we are uncertain about.

    We have no bibliographic references for this item. You can help adding them by using this form .

    If you know of missing items citing this one, you can help us creating those links by adding the relevant references in the same way as above, for each refering item. If you are a registered author of this item, you may also want to check the "citations" tab in your RePEc Author Service profile, as there may be some citations waiting for confirmation.

    For technical questions regarding this item, or to correct its authors, title, abstract, bibliographic or download information, contact: Chief Editor (email available below). General contact details of provider: https://www.carijournals.org/journals/index.php/ejl/ .

    Please note that corrections may take a couple of weeks to filter through the various RePEc services.

    IDEAS is a RePEc service. RePEc uses bibliographic data supplied by the respective publishers.