IDEAS home Printed from https://ideas.repec.org/a/bdu/ojtijl/v3y2022i1p1-19id1538.html
   My bibliography  Save this article

Taswira ya Jamii ya Kisasa kwa Mujibu wa Riwaya Teule za Kisasa za Mwandishi K.W. Wamitila

Author

Listed:
  • Janice M. Mutua

Abstract

Lengo: Makala hii inakusudia kuangazia taswira kamili ya jamii ya kisasa kama ilivyodhihirika katika riwaya mpya teule za Musaleo! na Mwandishi, Msomaji na Mchapishaji zilizoandikwa na K.W. Wamitila. Mwandishi amefanikiwa kuieleza jamii ya kisasa kupitia kwa usimulizi wenye simulizi nyingi fupi fupi ambayo ni kipengee kimojawapo cha mbinu ya utunzi ya kimajaribio. Mbinu ya utafiti: Mtafiti aliafikia lengo la utafiti kwa kutumia mbinu ya uchanganuzi wa yaliyomo mkabala wa ufasili. Mtafiti ameangazia maandiko yenye uhusiano na jinsi riwaya mpya ilivyoichorea hadhira taswira ya jamii husika. Kipengee cha kimajaribio kilichotumika ni matumizi ya simulizi fupi fupi zilizomo katika simulizi kuu. Data ya utafiti ilikusanywa maktabani kutoka katika uchambuzi wa maudhui katika riwaya za Musaleo! (ML) na Mwandishi, Msomaji na Mchapishaji (MMM). Nadharia ya Usasaleo kama ilivyoasisiwa na Jean Baudrillard iliuongoza utafiti katika ukusanyaji na uchanganuzi wa data. Matokeo: Utafiti umebaini kwamba ukosefu wa utaratibu katika utekelezaji wa shughuli mbali mbali uandishi ukiwemo, waweza kuonekana usiofaa lakini hiyo ndiyo taswira kamili ya maisha katika jamii ya kisasa; hayana utaratibu mahususi. Hali ya mparaganyiko imechukua nafasi kubwa ya maisha ya kisasa. Makala imebainisha kuwa jamii inakabiliana na changamoto nyingi. Aidha imeonyesha jinsi jamii yenyewe inavyojimudu kuzitatua. Mchango wa Kipekee kwa Mujibu wa Nadharia: Mintarafu ya nadharia, mwandishi bunifu ana uhuru wa kuandika jinsi apendavyo, hailazimu kwamba riwaya zifuate utaratibu mahususi. Hii ni kwa sababu maisha katika jamii ya kisasa hayana utaratibu wowote.

Suggested Citation

  • Janice M. Mutua, 2022. "Taswira ya Jamii ya Kisasa kwa Mujibu wa Riwaya Teule za Kisasa za Mwandishi K.W. Wamitila," International Journal of Linguistics, IPRJB, vol. 3(1), pages 1-19.
  • Handle: RePEc:bdu:ojtijl:v:3:y:2022:i:1:p:1-19:id:1538
    as

    Download full text from publisher

    File URL: https://iprjb.org/journals/IJL/article/view/1538
    Download Restriction: no
    ---><---

    More about this item

    Keywords

    ;
    ;
    ;
    ;

    Statistics

    Access and download statistics

    Corrections

    All material on this site has been provided by the respective publishers and authors. You can help correct errors and omissions. When requesting a correction, please mention this item's handle: RePEc:bdu:ojtijl:v:3:y:2022:i:1:p:1-19:id:1538. See general information about how to correct material in RePEc.

    If you have authored this item and are not yet registered with RePEc, we encourage you to do it here. This allows to link your profile to this item. It also allows you to accept potential citations to this item that we are uncertain about.

    We have no bibliographic references for this item. You can help adding them by using this form .

    If you know of missing items citing this one, you can help us creating those links by adding the relevant references in the same way as above, for each refering item. If you are a registered author of this item, you may also want to check the "citations" tab in your RePEc Author Service profile, as there may be some citations waiting for confirmation.

    For technical questions regarding this item, or to correct its authors, title, abstract, bibliographic or download information, contact: Chief Editor (email available below). General contact details of provider: https://iprjb.org/journals/IJL/ .

    Please note that corrections may take a couple of weeks to filter through the various RePEc services.

    IDEAS is a RePEc service. RePEc uses bibliographic data supplied by the respective publishers.